Karagwe FM

Kyerwa kuwafikia watoto 95,454 chanjo ya polio

19 September 2023, 3:44 pm

Watoto  95,454  wenye umri kuanzia 0 hadi miaka 8 wilayani Kyerwa watapatiwa chanjo ya Polio kuanzia September  21-24 mwaka huu.

Akizungumza na Redio Karagwe Fm  Sauti ya Wananchi September 19 mwaka huu, Mratibu wa Elimu ya Afya kwa Umma (DPH co) wilaya Kyerwa mkoani Kagera Bi. Cornelia T. Inyoma amesema ili kutekeleza maagizo ya serikali wazazi na walezi wenye watoto wenye umri kuanzia miaka 0 hadi  miaka 8 wanatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha  muda utakapo wadia kwani chanjo hizo zikitolewa kwa walengwa zitasaidia taifa la Tanzania kuwa na watoto wenye Afya njema.

Kushoto ni Bi Cornelia T. Inyoma (DHP co) wilaya Kyerwa

Aidha Bi. Inyoma amesema ili zoezi la uhamasishaji wa kampeini ya chanjo ya Polio katika wilaya ya Kyerwa liweze kufanyika kwa ufanisi ni vyema wahudumu wa Afya ngazi za vijiji (CHW) washirikiane kwa ukaribu na jamii wakati wote  ambapo kampeini hii inapoendelea wilayani humo.

Itakumbukwa kuwa Wizara ya Afya nchini, chini ya waziri wake Mhe. Ummy Mwalimu akiwa Jijini Dodoma alisema kuwa wizara yake kwa kushirikiana Ofisi ya Rais TAMISEMI na Wadau wa Sekta ya Afya  wataendesha Kampeni ya uchanjaji chanjo dhidi ya ugonjwa wa polio kwa watoto zaidi ya Milioni 3,250,598 walio chini ya miaka 8 kwenye Mkoa wa Rukwa, Kagera, Kigoma, Katavi, Songwe na Mbeya.

Sauti ya ( DHP co) wilaya Kyerwa Bi Cornelia T. Inyoma