Karagwe FM

28 wapigwa msasa kwa ajili ya Uokoaji

4 July 2023, 1:04 pm

Jumla ya Askari 28 wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji kutoka mikoa mbalimbali Nchini Tanzania wameshiriki mafunzo ya pamoja ili kujiongezea ujuzi utakaowasaidia wakati wa uokoaji yanapotokea majanga.

Akifungua mafunzo hayo Nov 21 mwaka huu,Kamishina msaidizi mwandamizi Zabrune Levson Muhumha,Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa Kagera amesema mafunzo hayo yatakuwa ni ya siku saba na yatasaidia pakubwa katika kuongeza ufanisi katika majukumu yao wakati wa Uokoaji yanapotokea majanga.

Naye mkaguzi msaidizi Piter Mbale, Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji wilaya ya Karagwe, akawashukuru  wafadhiri kutoka shirika la Europen Fire and Resque Support Association – Ujerumani

Kwa ufadhiri wao na akamshukuru Mbunge wa jimbo la Karagwe bwana Innocent Bashungwa kwa ushirikiano anaoutoa  kwao ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinazogusa maendeleo ya wananchi wa wilaya Karagwe,

Bwana Matthias Steinfort, Mkufunzi mkuu kutoka shirika la Europen Fire and Resque Support Association kutoka Ujerumani, Amesema licha ya kujisikia raha kuwa Karagwe, atatoa elimu kusudiwa kwa walengwa wote kwa muda wote uliopangwa kwasababu ni mtaalamu katika maswala ya zimamoto na uokoaji kwa miaka mingi sasa.

Nao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo yanayotolewa na wakufunzi kutoka shirika la Europen Fire and Resque Support Association, wakaahidi kuitumia vyema elimu watakayoipata na kwamba watakaporudi katika vituo vyao vya kazi watawafundisha  wenzao,