Karagwe FM

DC Karagwe aagiza kutaifisha kahawa badala ya faini

8 May 2024, 12:29 pm

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser akihutubia madiwani. Picha na Eliud Henry

Kumekuwa na tatizo la kuvuna na kuuza kahawa mbichi maarufu kama “Obutura “katika wilaya zinazolima zao hilo mkoani Kagera ikiwemo Karagwe. Hali hii inadaiwa kuwapunja wakulima kwani wanajikuta wakipata hasara kutokana na mauzo ya zao hilo kabla ya wakati wake.

Na. Catus Tito

Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Kalanga Laiser ameeleza kusikitishwa na uwepo wa madalali wanaojihusisha na ununuzi wa kahawa mbichi na kudai kuwa suala hilo linapunguza mapato ya halmashauri kwa kuwa biashara ya kahawa mbichi hufanyika kimagendo.

Alisema hayo Mei 7.2024 wakati akitoa taarifa ya serikali kwa baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe na kuwaagiza watendaji na madiwani kushirikiana na serikali kudhibiti magendo ya kahawa na kuwafilisi wote wanaokamatwa wakishiriki uvunaji na ununuzi wa kahawa mbichi kwani kitendo hiki kinapoteza mapato

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe wakifuatilia hoja zinazojadiliwa. Picha na Eliud Henry

Kupitia baraza hilo, mkuu wa wilaya akawataka madiwani kuisaidia serikali kukemea vitendo vya kujichukulia sheria mkononi ikiwemo ongezeko la vitendo vya mauaji na kujiua

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda akisisitiza jambo. Picha na Eliud Henry

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Wallace Mashanda akakiri uwepo wa vitendo vya uhalifu wilayani Karagwe na kuwataka maafisa tarafa na watendaji wa kata kufuatilia baadhi ya matukio yakiwemo ya michezo ya kamari maarufu kama mabonanza na mikopo umiza.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashuri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda