Karagwe FM

Mrajis wa vyama vya ushirika azindua miradi yenye thamani ya mil. 890 Karagwe

25 November 2023, 8:47 pm

Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Bara Dkt. Benson Otieno Ndiege (katikati) Akizindua fedha iliyotolewa kama mtaji anzia kwenye SACCOS iliyoanzishwa na Chama kikuu cha Ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU LTD: Picha na Eliud Henry

Na Eliud Henry

Karagwe

Mrajis na Mtendaji Mkuu Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dkt. Benson Ndiege, amezindua miradi ya Shilingi 899,123,987 iliyotekelezwa kwa fedha za ruzuku ya jamii zilizotokana na mauzo ya Kahawa Maalum kwa msimu wa mwaka 2022/2023 katika Chama Kikuu cha Ushirika cha Karagwe (KDCU).

Dkt. Ndiege amezindua na kugawa vitendea kazi ikiwa ni pamoja na Pikipiki 23 zilizogharimu Shilingi 64,400,000, Vishikwambi 40 vyenye thamani ya shilingi 37,600,000, Ununuzi wa mashuka 500 kwa ajili ya wodi ya kina mama iliyoghalimu Shilingi 11,720,650, Mtaji anzia wa SACCOS 150,000,000 na Mgao wa Vyama vya Msingi kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu kwa kiasi cha shilingi 225,000,000.

Katika hatua nyingine Dkt. Benson Otieno Ndiege amewaagiza warajisi wa vyama vya ushirika mikoa yote nchini kufanya ukaguzi wa fedha katika vyama vya ushirika ili kuhakikisha fedha za ushirika zinatumika ipasavyo katika miradi ya vyama hivyo.

Sauti ya Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Dakt. Benson Otieno Ndiege

Ameayasema hayo katika hafla ya uzinduzi wa miradi mbalimbali iliyotekelezwa na chama kikuu cha ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU LTD kwa fedha za ruzuku ya jamii kwa msimu wa 2022/2023 hafla iliyofanyika Novemba 24, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Bishop Mukuta mjini Kayanga.

Dkt. Ndiege amesema kuwa viongozi wote wa vyama ushirika hawana budi kuhakikisha wanarudisha imani ya wananchi kwa vyama vya ushirika kwa kufanya kazi kwa uaminifu ikiwa ni pamoja Kudumisha ushirikiano na wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali.

Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Dkt. Benson Otieno Ndiege

Katika hatua nyingine Ndiege amewapongeza viongozi wa KDCU LTD kwa kuwa na miradi mingi ya mfano na kuvitaka vyama vyingine vya ushirika kuiga mfano huo maana ndiyo malengo makuu ya ushirika.

Mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Bara Dakt. Benson Otieno Ndiege

Kwa upande wake mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM taifa Kareem Amri Amir amesema kuwa vyama vya  ushirika vikifanya vizuri vinasaidia pakubwa katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi inayotekelezwa na serikali inayoongozwa na Rais wa jamuhuri ya muunga wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Awali akisoma taarifa ya miradi ya iliyotekelezwa na KDCU LTD kwa fedha za ruzuku ya jamii msimu wa 2022/2023 kaimu meneja wa KDCU LTD Robert Domisian Kigunia amesema miradi iliyozinduliwa ni Pamoja na ugawaji wa pikipiki kwa maafisa Ugani wa KDCU kama anavyo sikika

Sauti kaimu meneja wa KDCU LTD Robert Domisian Kigunia

Kaimu mwenyekiti wa KDCU LTD Bwana Mertus Biduli wakati akifunga hafla hiyo amesema kuwa kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye jamii siyo hiari bali ni moja ya malengo ya chama hicho cha ushirika.

Na hawa hapa ni miongoni mwa wanufaika wa miradi iliyozinduliwa akitoa maoni yao na kueleza jinsi watakavonufaika na mradi wa SACCOS Unaolenga kuwakopesha wakulima ili kuondoa adha ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa bado yapo mashambani.