Karagwe FM

Maulidi kitaifa kuadhimishwa mkoani Kagera

29 September 2021, 6:44 am

Baraza kuu la waislamu Tanzania BAKWATA Makao makuu linatarajia kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad maarufu kama Maulidi mwaka huu kitaifa mkoani Kagera.

Sheikh wa mkoa wa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta

Akiongea na wandishi wa habari Septemba 28 mwaka huu Sheikh wa mkoa wa Kagera alhaji Haruna Kichwabuta amesema kuwa wamemwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya mazazi ya mtume Muhammad yatakayofanyika kitaifa mjini Bukoba Oktoba 18 na 19 mwaka huu.

Sheikh wa mkoa wa Kagera Alhaji Haruna Kichwabuta

Alhaji Kichwabuta amesema kuwa maulidi ya mwaka huu itasomwa mkoani Kagera baada ya kupita kipindi kirefu tangu maadhimisho haya kufanyika mkoani hapa na kwamba imebeba kauli mbiu ya Maulidi na Maendeleo ikiwa na maana ya kuhamasisha maendeleo eneo inapoadhimishwa.