Karagwe FM

Jitihada za wananchi kuwanusuru watoto wanaotembea km12 kufuata elimu ya msingi

3 September 2023, 5:42 pm

Ujenzi wa shule shikizi taraji ya Kashasha ulioanzishwa na wananchi ili kunusuru watoto wao wanaotembea umali mrefu kufuata shule iliyopo umbali zaidi ya Km 6, Picha na Eliud Henry

Asilimia kubwa ya watoto katika vitongoji 3 vya kashasha,mjunju na Bweranyange katika kata ya Bweranyange wilayani Karagwe wanashindwa kuendelea na masomo yao kutokana shule kuwa mbali jambo lililowafanya wananchi wa vitongoji hivyo kuanza ujenzi wa shule shikizi ili kuwanusuru watoto hao.

Na Eliud Henry

Karagwe

Wanachi wa vitongoji 3 vya kashasha,mjunju na Bweranyange wameanzisha shule shikizi ya Kashasha ili kuondoa changamoto ya watoto kutembea umbali mrefu Zaid ya kilometa 12 kufuata shule mama iliyopo Kijiji Kijumbula kata Bweranyange wilayani Karagwe.

Wananchi hao wamefikia hatua ya kujenga shule shikizi kutokana na uwepo wa watoto wengi wanaoshindwa kuendelea na masomo yao wakiwa wadogo huku wengine wakichelewa masomoni kutokana na shule zilizopo kuwa mbali ndipo wakaamua kuanzisha shule shikizi ya kashasha kwa nguvu zao iliyofikia usawa wa kuezeka ikiwa na vyumba viwili vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Karagwe Wallace Mashanda (Aliyesimama) Akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kijumbura wilayani Karagwe, Picha Na Eliud Henry

Akizungumza na wananchi wa kijji cha Kijumbura katika mkutano wa hadhara uliofanyika septemba mosi mwaka huu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe Wallace Mashanda amewapongeza wanachi Kwa jitihada hizo na kusema kuwa ni jumla ya shule shikizi 16 ambazo zimeanzishwa Kwa nguvu za wananchi wilayani Karagwe  hivyo kuwa nguvu za wananchi zinapoanzishwa na serikali inaweka nguvu Yake ili kumalizia mahitaji ya shule hizo.

Amesema halmashauri inayokazi kubwa kuziunga mkono shule zote shikizi zilizoanza Kwa nguvu ya wanachi huku shule kongwe zilizopo Nazo Zikiwa na mahitaji mbalimbali hivyo wanachi waendelee kuunga mkono jitihada za serikali na kuilinda miradi Yao ili idumu Kwa muda mrefu.

Aidha Mashanda amewaomba wananchi kuweka juhudi za kilimo na kuhakikisha wanalima mazao ya chakula Cha kulisha familiazao na ziada kupeleka shuleni Kwa ajili ya watoto wao wawapo shuleni ikiwa ni wajibu wa wazazi kutimiza majukumu Yao kwenye familia na kwenye jamii

Wananchi wa kijiji cha Kijumbura kata ya Bweranyange wilayani Karagwe, Picha na Eliud Henry

Katika hatua nyingine mashanda amewataka wananchi kubadili kilimo Cha zamani na kulima kisasa ili kuondokana na umasikini ambapo amesema kuwa mabadiliko ya teknolojia yaendane na mwitikio wa wanachi katika kilimo Cha kutumia mbegu Bora pamoja na kuzingatia matumizi bora ya wakati katika msimu wa kilimo na kuacha tabia ya kucheza kamari,kalata na unywaji pombe ,kwani vitu hivyo vimechangia umasikini katika familia na kushindwa kuchangia michango ya miradi mbalimbali katika maendeo Yao.