Karagwe FM

Wazee watakiwa kuchangamkia bima ya afya

10 September 2023, 8:53 pm

Wazee wa  kikundi cha Bikolw’engonzi kilichopo kata ya Bugandika wilayani Missenyi: Picha na Eliud Henry.

Na. Jovinus Ezekiel

Missenyi

Wazee katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kujiunga na bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma za matibabu.

Akiongea   na wazee wa  kikundi cha  wazee Bikolw’engonzi kilichopo katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi ambacho kinafadhiliwa na shirika la shina Inc lenye makao makuu nchini  marekani kwa kuwakutanisha wazee kwa pamoja ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kubadilishana mawazo.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bugandika Dr.Jesto Kisambale aliyesimama akitoa elimu kuhusu Bima ya Afya kwa wazee: Picha na Eliud Henry.

Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bugandika Jesto Kisambale amesema kuwa wazee hao pamoja na wazee wengine ambao hawako  katika kikundi hicho katani humo inabidi wajiunge na huduma ya bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.

Sauti ya Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bugandika Dr.Jesto Kisambale

Amesema kuwa endapo wazee watajiunga na bima hiyo itawasadia kunufaika na huduma ya matibabu toafuati na ilivyo sasa ambapo baadhi yawazee hawana bima.

Naye Bi. Jesca Kamala Mushala   rais wa shirika la shina Inc ambalo limejikita katika utoaji wa  Huduma kwa makundi mbalimbali ya wazee, watoto,wanawake na vijana katika nyanja mbalimbali za kuwajengea uwezo kiuchumi na kutoa huduma ya elimu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar amesema kuwa lengo la shirika hilo ni kuhakikisha wazee wa kikundi cha wazee Bikolw’engonzi wanapata bima.

Sauti ya Bi. Jesca Kamala Mushala rais wa shirika la shina Inc
Bi. Jesca Kamala Mushala   rais wa shirika la shina Inc akisalimiana na wazee wa kikundi Bikolw’engonzi wilayani Missenyi: Picha na Eliud Henry.

Hata hivyo nao baadhi ya wazee wa kikundi hicho Audax Mlokozi na Demetilia Pasikale wamesema  kuwa suala la kupata  bima ni muhimu kwao ili kunufaika na huduma za matibabu.

Sauti za wazee wa kikundi cha Bikolw’engonzi