Karagwe FM
Karagwe FM
13 May 2026, 15:06

Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ni miongoni mwa wilaya hapa mkoani Kagera ambazo zimekuwa zikiripotiwa kukumbwa na matukio ya vitendo vya ukatili kwa watoto
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe
Shirika la kuhudumia watoto na vijana wenye ulemavu wilayani Karagwe CBIDO kwa kushirikiana na wadau wa kupinga vitendo vya ukatili limejipanga kutokomeza vitendo hivyo katika jamii kupitia mradi wa wezesha mtoto.
Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera ni miongoni mwa wilaya hapa mkoani Kagera ambazo zimekuwa zikiripotiwa kukumbwa na matukio ya vitendo vya ukatili kwa watoto ambavyo wakati mwingine watoto hufanyiwa na watu wao wa karibu licha ya uwepo wa sheria ya mtoto ya 2009 inayotambulika kimataifa kumlinda mtoto.
Katika kutazama suala hilo kwa upana uongozi wa shirika la kuhudumia watoto na vijana wenye ulemavu wilayani Karagwe CBIDO umeanza kushirikiana na wadau kuendeleza jitihada za mradi wa wezesha mtoto kwa ufadhili wa Lilian Faundation kupitia mshirika mkuu Beyond Inclussion Tanzania ambao utashirikisha wadau ili kupinga vitendo vya ukatili kwa watoto kama anavyosema Donatus Kaihula kwa niaba ya mkurugenzi wa shirika la CBIDO wakati wa kikao cha pamoja kilichowakutanisha wadau hao pamoja uongozi wa shirika hilo katika ukumbi wa Benjamini eneo la Nyakanongo kata ya Kayanga.

Mkuu wa idara ya ustawi wa jamii wilayani Karagwe Owokusima Kaihula ameeleza jinsi ukubwa wa tatizo ulivyo kwa vitendo vya ukatili kwa watoto wa wilaya hii kwa kutoa takwimu.

Baadhi ya wadau walioshiriki kikao hicho akiwemo mwenyekiti wa mamlaka ya mji mdogo wa Kayanga Projest Kajuna na Iginas Rugemarila mwenyekiti wa chama cha watu wenye ualbino wilayani Karagwe wametoa maoni yao ambapo pia afisa ustawi wa jamii katika shirika la CBIDO anaami kuwa mradi wa wezesha mtoto utaleta tija katika jamii.