Karagwe FM

I.P.I yajizatiti kulinda amani kwenye uchaguzi

4 April 2025, 20:21

Rais wa taasisi ya Umoja wa Amani kwanza taifa Prof Wilson George Munguza. Picha na Theophilida Felician

Wakati joto la uchaguzi mkuu likiendelea kupanda nchini wananchi wametakiwa kuungana pamoja kudumisha na kulinda amani wakati wa uchaguzi huo

Na Theophilida Felician.

Taasisi ya umoja wa amani kwanza nchini I.P.I imeeleza kuwa katika kuelekea kipindi cha uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na Udiwani imejipanga vilivyo ili kueneza elimu ya kutunza na kudumisha amani kwa wananchi.

Ameyasema hayo Rais wa taasisi hiyo taifa Prof Wilson George Munguza April 4, 2025 akiwa makao makuu ya ofisi za taasisi hiyo Temeke Mkoani Dar es Salaam akisema taasisi hiyo imejiandaa vya kutosha kuwafikia wananchi kwa malengo ya kuwaelimisha umuhimu wa kuitunza amani nyakati zote za uchaguzi kama ilivyo siku zote.

Rais wa taasisi ya Umoja wa Amani kwanza taifa Prof Wilson George Munguza
Rais wa taasisi ya Umoja wa Amani kwanza Zanzibar Dr Mohamed Said Ramadhan. Picha na Theophilida Felician

Naye Rais wa taasisi hiyo kwa upande wa Zanzibar Dr Mohamed Said Ramadhan amesema kuwa amani hii iliyodumu kwa muda mrefu ni vyema kila mmoja akaendelea kuwa askari wakuilinda muda wote iwe ni kipindi cha chaguzi na baada ya chaguzi.

Rais wa taasisi ya Umoja wa Amani kwanza Zanzibar Dr Mohamed Said Ramadhan