Karagwe FM
Karagwe FM
1 May 2026, 3:22 pm

Akwilina: “Tumalize migogoro yetu wenyewe, tusimkaribishe mtu mwingine kujua hata kama tuna changamoto”
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe
Wanachama wa chama cha ushirika Buhamila Amcos kilichopo katika kata ya Rugera wilayani Karagwe mkoani Kagera wametakiwa kuungana pamoja kuendeleza ushirika huo ili wapate faida ya pamoja.
Akizungumza na wanachama waliokusanyika katika hafla ya kupokea cheti cha usajili eneo la shule ya msingi Nyarugando kata ya Rugera afisa ushirika wa wilaya ya Karagwe Akwilina Meela amewataka wanachama na viongozi wa bodi kushirikiana katika utatuzi wa changamoto na utendaji kazi ili wafanikiwe pamoja na kufurahia matunda ya ushirika huo

Naye katibu wa chama cha ushirika Buhamila Amcos Finias Fildolin Fillipo wakati akisoma taarifa kwa niaba ya mwenyekiti wa ushirika huo amesema kuwa wanakusudia kuongeza thamani ya mazao kupitia mbinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao
Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa ushirika wa Buhamila Amcos amesema kuwa ushirika huo wenye wanachama 70 hivi sasa unanunua kahawa kwa bei elekezi ya serikali na kwamba bado wanahitaji wanachama hata wa maeneo ya nje ya kata ya Rugera