Karagwe FM

TAMESO (T) waomboleza kifo cha Ndugai

8 August 2025, 20:11

Kifo cha mwanasiasa mkongwe na spika mstaafu Job Ndugai kimewagusa watu wengi wakiwemo waganga wa tiba asili nchini hasa wanachama wa TAMESO Tanzania

Na Theophilida Felician.

Chama cha waganga wa tiba asili nchini TAMESO (T) kimeelezea kuguswa na kifo cha spika mstaafu Job Yustino Ndugai kutokana na alivyokuwa na mchango mkubwa kwa chama hicho tangu akiwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Yameelezwa hayo na Katibu mkuu wa chama hicho Bw Lukas Joseph Mlipu wakati akizungumza na Radio Karagwe kwa njia ya simu akiwa Mbarali mkoani Mbeya katika ziara ya kuhamasisha wiki ya tiba asili ya mwafrika ambapo amesema kwa niaba ya wanachama wenzake wameupokea kwa masikitiko makubwa msiba wa kiongozi huyo aliyefariki Agosti 6. 2025 mkoani Dodoma.

Katibu mkuu Lukasi amefafanua kwamba Marehemu Job Ndugai alikuwa ni mchango mkubwa kwa chama kwani alitoa ushauri wa karibu na wenye kukijenga, aliwahi kuwa msaada kwa chama baada ya kukisaidia mawazo yenye kuutatua mgogoro uliokuwa ndani ya chama mwaka 2018 na kutatuliwa 2019 kipindi hicho akiwa spika wa Bunge.

Katibu mkuu wa chama hicho Bw Lukas Joseph Mlipu