Karagwe FM

Waajiri wasiolipa watumishi kwa wakati Kagera kuchukuliwa hatua

2 May 2026, 10:05 am

Malalamiko ya wafanyakazi nchini juu ya mazingira duni ya kazi imekuwa kilio chao kila wanapoadhimisha siku ya wafanyakazi duniani hasa wakiiomba serikali kuchukua hatua kwa waajiri

Na Respicius John, Missenyi

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido amewaagiza waajiri katika sekta binafsi kulipa kwa wakati mishahara ya watumishi wao kulingana na kima cha chini cha msahara kilichotangazwa na serikali sambamba na kuwasainisha mikataba ya hali bora ya kazi

Kanali Kido ametoa maagizo hayo wakati akihutubia maelfu ya wafanyakazi wa mkoa wa Kagera wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei mosi yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya kiwanda cha sukari Kagera

Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Yahya Ramadhan Kido

Katika risala ya wafanyakazi iliyosomwa na mratibu wa shirikisho la wafanyakazi TUCTA mkoa wa Kagera Njile Antony imebainisha changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kagera ikiwa ni pamoja na mishahara duni kwa watumishi wa sekta binafsi

Mratibu wa shirikisho la wafanyakazi TUCTA mkoa wa Kagera Njile Antony
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Missenyi wakiwa katika maadhimisho ya Mei mosi. Picha na Respicius John
Viongozi wakuu mkoa wa Kagera wakiwa meza kuu wakati wa maadhimisho ya Mei mosi eneo la Kagera sugar. Picha na Respicius John