Karagwe FM

‘Greening Karagwe Project’ kudhibiti nishati chafu Karagwe

8 May 2024, 9:37 pm

Afisa maliasili na mazingira bw. Rajab Kassim. Picha na Eliud Henry

Kampeni kabambe kwa sasa hapa nchini ni ulinzi wa mazingira kwa kudhibiti ama kupunguza matumizi ya nishati chafu yaani kuni na mkaa. Afisa maliasili na mazingira wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera bw. Rajab Kassim akishirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali anaamua kuja na mradi wa kutengeneza Karagwe ya kijani kwa kubuni nishati mbadala ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa

Na Catus Tito

Halmashauri ya wilaya ya Karagwe  mkoani Kagera kwa kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali imetambulisha mradi wa uhifadhi wa mazingira (Greening Karagwe Project) utakaogharimu zaidi ya shilingi bilioni sita.

Afisa Maliasili na mazingira wilaya ya Karagwe bw. Rajab Kassimu akitambulisha mradi huo wa uhifadhi wa mazingira (Greening Karagwe Project) kupitia mkutano wa baraza la madiwani wa halmshauri ya wilaya ya Karagwe wa robo ya tatu ya mwaka 2023/2024   Mei 7, 2024  amesema kuwa kwa kushirikiana na wadau halmashauri imekuja na mradi huo ili kutatua kero za uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na kutengeneza mkaa mbadala kufuatia tangazo la serikali la katazo la taasisi zote zenye watu zaidi ya mia moja kutotumia kuni na mkaa

Sauti ya afisa maliasili na mazingira bw. Rajab Kassim

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Karagwe wakiwa katika kikao

Wakitoa mchango wao kuhusu mradi huo baadhi ya madiwani akiwemo diwani wa kata ya Nyakabanga Jastine Tinkaligayile Fidelis, Zidina Murshid wa kata ya Kituntu na Adrian Kobushoke wa kata ya Rugu wameipongeza halmashauri na wadau waliokubaliana kuanzisha mradi huo wakisema kuwa utachangia pakubwa katika ulinzi wa mazingira

Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Karagwe wakichangia hoja ya kuanzishwa kwa mradi wa Greening Karagwe