Karagwe FM

Vyombo vya habari Kagera kuchochea miradi ya maendeleo

22 September 2023, 5:45 pm

Washiriki wa warsha iliyoandaliwa na shirika la maendeleo ya petroli Tanzania TPDC

Mradi wa bomba la mafuta ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali unaohusisha nchi mbili kwa  maana ya Tanzania na Uganda hivyo waandishi wa habari hawana budi kueleza wananchi habari sahihi na kwa wakati juu ya mwenendo wa mradi huo.

Na Ospicia Didace

Serikali ya wilaya ya Bukoba imevitaka vyombo vya habari mkoani Kagera , kuendelea kufuatilia miradi na shughuli zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita inayolenga kukuza uchumi wa nchi na wananchi kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wa habari juu ya mwenendo wa  mradi wa kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga Tanzania.

Amesema kuwa mradi wa bomba la mafuta ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na serikali na kwamba mradi huo unahusisha nchi mbili kwa  maana ya Tanzania na Uganda hivyo waandishi wa habari hawanabudi wakueleza wananchi habari sahihi na kwa wakati juu mwenendo wa mradi huo.

Bwana Siima ameongeza kuwa zipo taarifa ambazo ofisi yake imekuwa ikipata kuhusu migogoro ya kifamilia  kuhusu ulipaji wa fidia kwa watu wanaopitiwa na mradi huo, kutokana na kuwepo kwa migogoro ya kifamilia ya umiliki wa ardhi husika na migogoro hiyo imekuwa ikimalizwa kifamilia.

Amesisitiza umuhimu wa vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu mradi huo ,Ili kuepusha migogoro ya namna hiyo na kufikiwa kwa lengo la serikali.

“Uzalishaji wa gesi asilia una faida kubwa kwa wananchi kwani unachangia nishati ya umeme kwenye gridi ya Taifa asilimia 75 ambapo nishati hiyo inatumiwa na watanzania katika shughuli mbalimbali za kuinua uchumi”

Aidha imeelezwa kuwa mpaka sasa zaidi ya asilimi 90 ya fidia imetolewa kwa walengwa na mradi umeanza kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika ifikapo 2025.

Katika semina hiyo imeelezwa kuwa Wananchi  wa mikoa nane ya Tanzania unapopitia mradi wa bomba la mafuta (EACOP) hawana budi kushiriki katika  fursa mbalimbali kama huduma za chakula na kazi zisizo hitaji ujuzi yaani vibarua.

Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta East African Crude Pipeline (EACOP) Bw. Abass Abraham

 Afisa mahusiano wa mradi wa bomba la mafuta East African Crude Pipeline (EACOP) Abass Abraham amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unaendelea  ukitarajiwa  kutoa ajira 6000 za kudumu na zile za muda ambapo mpaka sasa wametoa asilimia 99 ya fidia kwa wananchi wanaopitiwa na mradi huo sambamba na kujenga nyumba 124 kwa wanaliovunjiwa nyumba zao mkoani Kagera.

Meneja mahusiano wa shirika la maendeleo ya petroli Tanzania TPDC Bi.Marie  Msellemu

Marie  Msellemu ni meneja mahusiano wa TPDC  amesema uzalishaji wa gesi asilia una faida kubwa kwa wananchi kwani unachangia nishati ya umeme kwenye gridi ya Taifa asilimia 75 ambapo nishati hiyo inatumiwa na watanzania katika shughuli mbalimbali za kuinua uchumi.