Karagwe FM

DC Karagwe awakalia kooni askari wala rushwa

16 April 2024, 1:18 am

Dc Karagwe Julius K.Laizer akizungumza na wananchi katika Mkutano Nyakaiga – Karagwe

Rushwa ni adui wa haki, utu, heshima na haki msingi za binadamu hivyo jamii lazima ishiriki vyema kuitokomeza

Na Devid Geofrey:

Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Kalanga Laizer amepiga marufuku vituo vya polisi kuwatoza  wananchi fedha kwa madai ya kumfata mtuhumiwa huku akibainisha kuwa jukumu la jeshi la polisi kumtafuta muhalifu bila malipo.

Agizo hilo limetolewa kupitia mkutano uliofanyika hivi karibuni katika tarafa ya Nyakakika katika ofisi ya kata Nyakaiga April 2 mwaka huu kwa lengo la kusikiliza kero za mwananchi na kuzitafutia majibu

Baadhi ya wananchi wa Nyakaiga wakimsikiliza mkuu wa wilaya wakati wa maswali na majibu. Picha na Eliud Henry

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kusikitishwa na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya askari polisi wilayani humo kuwataka wanachi kulipia pesa kwaajili ya nauli ya kuwakamata watuhumiwa kitendo ambacho amesema ni kinyume na sheria za nchi.

Hata hivyo kupitia mkutano huo,Mkuu huyo wa wilaya amewaagiza makatibu tarafa kuhakikisha wanasimamia ofisi na taasisi zilizoko kwenye maeneo yao ya utawala ili ziweze kuwahudumia wananchi kazi kwa weledi na kwa wakati.

sauti ya Dc Karagwe Julius Laizer pamoja na Wananchi

Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa endapo wataombwa rushwa kwa lengo la kupatiwa huduma na akasema kwakufanya hivi itasaidia kukomesha vitendo hivyo vinavyofanywa na baadhi ya watu wasio waadilifu.