Karagwe FM

Bilioni 82 zatengwa kwa ajili ya miradi.

28 April 2021, 2:40 pm

Manispaa ya Mji wa Bukoba imetenga jumla ya shilingi bilioni 82 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayosaidia kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya wananchi.

Wa kwanza kushoto ( Mstahiki Meya Manispaa ya Bukoba Godson Rwegasila Gypson)

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Godson Rwegasila Gypson ambaye pia ni diwani wa kata ya Nshabya alipokuwa akizungumza na Redio Karagwe fm sauti ya wananchi April 27 mwaka huu.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Godson Rwegasila amesema kwa sasa kinachoendelea ni kuweka mikakati mathubuti itakayo mwezesha kufikia malengo.

Mstahiki Meya (Manispaa ya Bukoba Godson Rwegasila Gypson)