Karagwe FM

TCRA yawaasa wafanyakazi Karagwe FM kuongeza ubunifu

20 April 2024, 9:30 pm

Meneja wa mamlaka ya mawasiliano Kanda ya Ziwa Mhandisi Imelda Salumu Banali (aliyesimama) akiongea na wafanyakazi wa Radio Karagwe. Picha na Eliud Henry

Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano umeendelea kwa kasi ya hali ya juu na kusukuma juhudi za watendaji kwenye vyombo vya habari kusaka ubunifu wa kupata ufuasi na masoko.

Na Shabani Ngarama

Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhandisi Imelda Salum Banali amewaasa wafanyakazi wa Redio Karagwe kuongeza ubunifu ili kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia.

Amesema hayo April 20, 2024 wakati akiongea na watangazaji wa Radio Karagwe na kuwasisitiza kuachana na tabia za kuiga utangazaji wa watangazaji wa vyombo vingine na badala yake wajitengenezee umaarufu kupitia ubunifu na kuiaminisha jamii kuwa wanaweza kutengeneza maudhui mazuri kama wakongwe wengine.

Mhandisi Imelda Salum Banali akiongea na wafanyakazi wa Radio Karagwe

Timu ya wataalam kutoka TCRA Kanda ya Ziwa waliotembelea Redio Karagwe.

Mhandisi Imelda pia amewataka wafanyakazi kujiandaa kuripoti habari za uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu mwaka ujao sambamba na kuahidi kushirikiana na vituo kuwapatia mafunzo fursa itakapopatikana.

Sauti ya Mhandisi Imelda Salum Banali akisisitiza wandishi kujiandaa kuripoti chaguzi

Baadhi ya wafanyakazi wa Redio Karagwe wakifurahia jambo kutoka kwa Mhandisi Imelda. Picha na Eliud Henry

Mkurugenzi wa Radio Karagwe Mch. Dk. Godfrey Aligawesa (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na baadhi ya watangazaji. Picha na Eliud Henry