Karagwe FM

Karagwe: DC aridhishwa utekelezaji wa miradi ya elimu

4 July 2023, 11:18 am

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser akiwa katika shule ya msingi Kambarage iliyopata fedha za mradi wa boost: Picha na Eliud Henry

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser amekagua na kuridhishwa na ujenzi wa vyumba vya madarasa chini ya mradi boost katika kata mbalimbali wilayani humo

Na, Shabani Ngarama

Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Kalanga Laizer ameridhishwa na utekelezaji wa miradi ya vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali wilayani hapa vilivyojengwa kwa fedha za serikali kupitia mradi wa BOOST.

Mradi umetekelezwa vizuri ikiwemo ukamilifu wa shule mpya ya Ahakarama ikiwa na vyumba 16 vya madarasa na matundu 24 ya vyoo

Akizungumuza na waandishi wa habari baada ya ukaguzi wa vyumba vya madarasa vilivojengwa kupitia mradi wa BOOST, mkuu wa wilaya Karagwe bw.Laizer amesema kuwa katika vyumba vya madarasa vilivyokaguliwa katika shule za msingi Omukakajinja kata ya Rugera,Nyakahanga kata ya Nyakahanga, Akarama kata ya Kanoni, Masheli kata ya Nyakakika Rwentue kata ya Nyabiyonza, Nyalugando kata ya Rugera pamoja na Rumanyika na Kambarage kata ya Kayanga ujenzi wake ni wa kuridhisha.

Kwa mujibu wa afisa elimu vifaa na takwimu anayeratibu mradi wa boost Dickson Zephrine amesema kuwa mradi huo umetekelezwa vizuri ikiwemo ukamilifu wa shule mpya ya Ahakarama ikiwa na vyumba 16 vya madarasa na matundu 24 ya vyoo.
Hata hivyo diwani wa kata ya Kayanga yalipo makao makuu ya wilaya ya Karagwe Germanus Byabusha ameishukuru serikali iliyowezesha mradi ya elimu katika kata yake katika shule mbili za msingi kwani shule zilizonufaika zilikuwa na uhitaji mkubwa wa vyumba vya madarasa na matundu ya vyoo sambamba na miundombinu ya watoto wenye ulemavu

Sauti ya Diwani wa kata ya Kayanga Germanus Byabusha

Moja ya vyoo vilivyojengwa chini ya mradi wa boost: Picha na Eliud Henry