Karagwe FM
Karagwe FM
8 August 2024, 21:32

Mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF mkoa wa Kagera umeripotiwa kukumbwa na ubadhirifu wa kutokana na uwepo wa baadhi ya watumishi wasio waaminifu waliokasimiwa mamlaka ya kusimamia mpango huo.
Na Theophilida Felician.
Katibu mkuu wa chama cha ACT wazalendo Ado Shaibu amesikitishwa na watu wanaofanya ubadhirifu wa fedha za mpango wa kunusuru kaya masikini TASAF maeneo mbalimbali hapa nchini na kuitaka serikali kufanya uchunguzi.
Shaibu ametoa kauli hiyo Agosti 7, 2024 wakati akiwahutubia wananchi wa manispaa ya Bukoba katika kata ya Rwamishenye na kuongeza kuwa ipo changamoto kubwa ya ubadhirifu wa fedha hizo za wanufaika wa mpango huo ambao unawelenga wananchi masikini.
Ameeleza kwamba tatizo hilo amelikuta maeneo mengi mikoa kadhaa alikopita katika ziara yake hivyo ameshangazwa kuona na Bukoba linajitokeza baada kupokea taarifa ya viongozi wa chama mkoa na jimbo.
Hata hivyo suala la hali ya umasikini kwa mkoa Kagera hakusita kulielezea kwa kuwa kiwango cha pato kiko chini ukilinganisha na takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa mara kwa mara na benki kuu ya Tanzania.
Amesema Kagera ni mkoa uliokaliwa rasirimali za kutosha hivyo haupaswi kuendelea kuwa kwenye orodha ya mikoa inayoshika nafasi ya mwisho kwa umakini.

Nao viongozi wa chama jimbo na mkoa akiwemo mwenyekiti wa mkoa Evodiu Justinian amezitaja kero kadhaa ikiwemo ya changamoto zinazojitokeza kwenye vituo vya kuandisha daftari la wapiga kura hasahasa ugomvi wa makada wa vyama vya siasa CCM na CHADEMA wakiwabagua baadhi ya watu kutokuandikishwa, kodi kubwa kwa wafanyabishara wadogo, wingi wa vizuizi (belia) barabarani na zaidi ubadhirifu wa miradi ya TASAF.
Viongozi hao wametoa angalizo kwa mkuu wa polisi wilaya ya Bukoba kutokufumbia macho chokochoko hizo kwani zinaweza kuleta uvunjivu wa amani kama hazitodhibitiwa.