Karagwe FM

Askofu Dkt. Bagonza atoa ujumbe mzito kwa wachungaji wapya

10 December 2023, 10:27 pm

Mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko aliyevaa suti akiwa na maaskofu waliohudhuria ibada ya kutabaruku Kanisa Kuu la Dayosisi ya Karagwe: Picha na Eliud Henry

Na Eliud Henry

Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe Mchungaji Dkt. Benson Kalikawe Bagonza amewataka wachungaji waliobarikiwa kutofanya maamuzi wakiwa na Hasira na kuwasisitiza kusikia kile ambacho wengine hawawezi kusikia.

Amesema hayo Desemba 10 mwaka huu katika Ibada ya Kutabaruku Kanisa Kuu la Dayosisi ya Karagwe lililopo katika usharika wa Lukajange kata ya Bugene iliyoambatana na ubarikio wa wachungaji watano katika Dayosisi hiyo na kufanya Idadi ya wachungaji walio hai 105 katika Dayosisi hiyo.

Sauti ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe Mchungaji Dkt. Benson Kalikawe Bagonza

Aidha, wachungaji waliobarikiwa wakapata nafasi ya kusema neno la Shukrani.

Sauti za wachungaji waliobarikiwa wakitoa neno la Shukrani.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika tendo hilo la Baraka Naibu Waziri Mkuu na waziri wa nishati Dk. Dotto Biteko aliyemwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Dayosisi ya Karagwe kipekee kwa kumpa nafasi ya kushiriki zoezi la Kutabaruku kanisa.

Sauti ya mgeni rasmi Naibu Waziri Mkuu na waziri wa nishati Dk. Dotto Biteko

Hata hivyo, tendo hili la Kutabaruku kanisa limehudhuriwa na Baba Maaskofu wa KKKT, Roman Catholic na viongozi wa kitaifa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Tanzania bara Bw. Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ujenzi Bw. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya.

Maaskofu pamoja na viongozi wa Serikali waliohudhuria Ibada ya kutabaruku Kanisa Kuu la Dayosisi ya Karagwe: Picha na Eliud Henry