Karagwe FM

Maadhimisho miaka 60 ya Muungano yaanza Missenyi

23 April 2024, 1:53 pm

Mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamisi Mayamba Maiga (aliyevaa suti meza kuu)

Picha na Respicius John

Shamrashamra za kuadhimisha miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zimeanza rasmi kote nchini kwa namna tofauti ambapo baadhi ya maeneo wamezindua maadhimisho hayo kwa dua na sala kwa ajili ya kuliombea taifa sambamba na kushiriki usafi na upandaji miti kwa ajili ya kutunza mazingira.

Na Rspicius John

Baadhi ya viongozi wa dini wilayani Missenyi mkoani Kagera wameungana na viongozi wa chama na serikali kufanya sala na dua kwa ajili ya kumuomba Mwenyezi Mungu adumishe amani na kuwapa afya njema viongozi wakuu wa serikali zote mbili yaani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar.

Baadhi ya washiriki katika hafla ya sala na dua kuashiria uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano

Picha na Respicius John

Akiwa katika hadhara ya maombi iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Missenyi katibu wa chama cha mapinduzi CCM Bakari Mwacha amewataka watanzania kuendelea kuulinda Muungano wetu na kudumisha amani huku kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi bi Tapita Solomoni akiamni kuwa maombi yaliyoanyika yatasaidia kudumisha Muungano

Sauti ya kaimu mkurugenzi mtendaji wilaya ya Missenyi bi Tapita Solomoni na katibu wa CCM wilaya ya Missenyi Bakari Mwacha

Baadhi ya viongozi wa dini walioongoza dua na sala kuliombea Taifa

Picha na Respicius John

Mgeni rasmi katika maombi haya alikuwa mkuu wa wilaya ya Missenyi kanali mstaafu Hamisi Maiga ambaye amewashukuru viongozi wa dini na wote walioshiriki kufanikisha maombi ya kuliombea taifa na kuwataka watendaji serikalini kuuenzi muungano kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu

Sauti ya Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanal Hamis Maiga