Karagwe FM
Karagwe FM
17 October 2026, 18:41

Mkuu wa kitengo cha trafiki kutoka jeshi la polisi wilaya ya Ngara mkoani Kagera amewaasa vijana na makundi mengine ya wananchi kujiunga na chuo cha mafunzo ya udereva ili kupata vyeti na leseni zitakazowawezesha kuendesha vyombo vya moto kwa kufuata sheria za usalama barabarani
Na Shabani Ngarama, Ngara-Kagera
Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi VETA Redeso kilichopo wilayani Ngara kimefanya mahafali ya kwanza yakihusisha wahitimu 12 wa udereva waliotunukiwa cheti na leseni za udereva katika viwanja vya posta mjini Ngara mkoani Kagera
Mgeni rasmi katika mahafali hayo mkuu wa kitengo cha usalama barabarani wilaya ya Ngaara SP Noel Kagosso amemshukuru mkurugenzi wa chuo hicho kwa kutoa nafasi ya mafunzo kwa makundi mbalimbali ya wananchi wakiwemo wazee wanaotafuta ujuzi wa ziada hasa katika fani ya udereva
Pia ameahidi kutumia mikutano yake kukitangaza chuo hicho ili kuhamasisha umma kuchukua mafunzo chuoni hapo ili kuongeza idadi ya madereva wenye ujuzi stahiki
