Karagwe FM

CHADEMA Kagera waahidi kupambania katiba mpya na demokrasia

3 September 2026, 23:18

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera Mwl Gratian Mukoba (wa kwanza kulia) akiwa katika kikao maalum wilayani Karagwe. Picha na Jovinus Ezekiel

Viongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoa wa Kagera wameweka maazimio kadhaa yanayolenga kuendeleza mapambano ya kutafuta katiba mpya na uhuru wa kisiasa

Na Jovinus Ezekiel, Karagwe

Uongozi wa chama Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Kagera umeahidi kuendeleza juhudi za kupambania watanzania kupata katiba mpya ambayo baadhi ya watanzania wanatamani kuona inapatikana. Akizungumuza na Radio Karagwe Septemba 2.2026 mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja cha mashauriano kilichofanyika mjini Kayanga wilayani Karagwe mkoani Kagera kwa kuwajumuisha viongozi wa nafasi mbalimbali za uongozi wa CHADEMA katoko wilaya za mkoa wa Kagera, mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kagera ameeleza lengo la kikao hicho.

Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera Mwl Gratian Mukoba
Baadhi ya wanachama na viongozi wa CHADEMA mkoa wa Kagera walioshiriki kikao maalumu wilayani Karagwe. Picha na Jovinus Ezekiel

Kwa upande wa wawakilishi wa CHADEMA ngazi ya wilaya na mkoa wamesema kuwa kutokana na chama hicho kuendelea kuaminiwa na wananchi wana jukumu la kuendeleza harakati za utetezi ikiwa ni pamoja na kudai uhuru wa kisiasa na kuelimisha wanachama kuachana na uoga

Baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoa wa Kagera
Jopo la viongozi wa CHADEMA mkoa wa Kagera wakiwa katika kikao maalum wilayani Karagwe. Picha na Jovinus Ezekiel