Karagwe FM
Karagwe FM
21 September 2026, 11:48

Shule ya awali na msingi ya kiingereza Hosiana iliyopo wilaya ya Karagwe mkoani Kagera imekuwa mfano wa kuigwa katika kuunga mkono kampeni matumizi ya nishati safi kwa taasisi zinazotoa huduma kwa zaidi ya watu 100 kama inavyoelekezwa na ofisi ya mkamu wa Rais Muungano na mazingira
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe
Katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais Dkt Richard Muyungi amepongeza uongozi wa shule ya awali na msingi ya kiingereza Hosiana iliyoko kata ya Ndama wilayani Karagwe mkoani Kagera kwa kubuni mradi wa nishati safi ya kupikia ili kuendeleza kampeni ya utunzaji wa mazingira.
Ni Furaha ya wahitimu wa darasa la saba 2026 katika shule ya kiingereza ya awali na msingi Hosiana iliyoko katika kata ya Ndama wilayani Karagwe wakionyesha furaha hiyo kwenye mahafali ya kuwaaga wahitimu hao yaliyofanyika Septemba 19.2026 shuleni hapo kwa kujumuisha uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa sekondari.
Katika risala ya wahitimu ambayo imesomwa kwa niaba yao na Renifa Raji imebainisha mafanikio ambayo wameyapata shuleni hapo ambapo hata hivyo mwalimu mkuu wa shule ya kiiingereza ya awali na msingi Hosiana Reont Kasasila katika taarifa yake amebanisha uwepo wa miundo mbinu rafiki katika shule ya Hosiana kuwa ni pamoja na uwepo wa nishati safi ya kupikia chakula cha wanafunzi.

Isaya Tendega kwa niaba ya katibu tawala wa mkoa wa Kagera amesema kuwa serikali ya mkoa wa Kagera itaendelea kushirikiana na shule hiyo katika kukuza maendeleo ya sekta ya elimu mkoani Kagera.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambayo ni sita kwa wahitimu wa darasa la saba shule ya kiiingereza Hosiana katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais Dkt Richard Muyungi amepongeza uongozi wa shule kwa kubuni mradi wa Nishati safi ya kupikia.
Kuhusu mradi wa shule ya sekondari mpya ya Hosiana akahimiza wanafunzi walihotimu darasa la saba shuleni hapo kupewa kipaumbele.

Mkurungezi wa shule ya Hosiana Shadrack Ntimba ambaye pia ni diwani wa kata ya Ndama kando ya mahafali hayo amesema kuwa mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ambao umezinduliwa na katibu mkuuu ofisi ya makamu wa Rais Dkt Richard Muyungi umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja ambapo pia baadhi ya wanafunzi waloiohitimu darasa la saba 2026 walieleza mafanikio
