Karagwe FM
Karagwe FM
29 August 2026, 22:09

Shirika la kuhudumia vijana na watoto wenye ulemavu mkoani Kagera CBIDO limeendelea kupanua mtandao wa ushirikiano na taasisi za serikali katika utoaji elimu ya kuzuia ulemavu
Na Jovinus Ezekiel, Karagwe
Uongozi wa shirika la kuhudumia watoto na vijana wenye ulemavu wilayani Karagwe CBIDO umeahidi kuendeleza mkakati wa kutoa elimu kwa walimu wa shule zenye vitengo vya elimu maalum hali itakayosaidia kutatua baadhi ya changamoto zinazokabili kundi hilo.
Akizungumuza Agosti 28. 2026 mara baada ya kumalizika kikao cha pamoja kilichowajumuisha baadhi ya walimu wakuu na walimu wanaofundisha shule zenye vitengo vya watoto wenye mahitaji maalum katika ukumbi wa mikutano Benjamini Hall uliopo Nyakanongo kata ya Kayanga wilayani Karagwe, mratibu wa shughuli za shirika la CBIDO Julieth Aloyce amesema kuwa lengo la kikao hicho ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Benjamin All mjini kayanga ni kuweka mpango mkakati wa kuwajengea uwezo walimu wanaofundisha shule zenye wanafunzi wenye mahitaji maalum ili kubaini baadhi ya changamoto zinazowakabili na jinsi ya kuzitatua.

Naye Merrynes Alphonce afisa elimu maalum idara ya elimu msingi halmashauri ya wilaya Karagwe anaamini kuwa elimu ambayo imetolewa italeta tija kubwa kwa walimu hao huku baadhi ya washiriki wa kikao hicho wakishukuru kwa elimu waliyoipata.
