Karagwe FM

Miradi 6 ya maendeleo kupitiwa na Mwenge wa uhuru Karagwe

28 August 2026, 12:33

Mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser. Picha na Shabani Ngarama

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kukimbizwa kilomite 50.5 wilayani Karagwe siku ya Ijumaa Septemba 4. 2026 ambapo pamoja na miradi mingine utazindua ghala la kahawa la kiwanda cha chama kikuu cha ushirika KDCU Ltd wilayani Karagwe mkoani Kagea

Na Shabani Ngarama, Karagwe

Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa Septemba 4. 2026 wilayani Karagwe ukitokea wilaya ya Kyerwa na kukimbizwa ukipita katika miradi sita ya maendeleo iliyotekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.9 ikiwa ni pamoja na mradi wa ghala la kiwanda cha kahawa la chama kikuu cha ushirika KDCU Ltd litakalozinduliwa siku hiyo

Mkuu wa wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Julius Laiser amesema kuwa mapokezi ya mwenge yatafanyika katika eneo la Maya kata ya Nyabionza baada ya mkesha wa mapokezi na kwamba utapita katika mradi wa kituo cha afya Nyabionza kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser
Baadhi ya wajumbe wa kamati ya Mwenge wilaya ya Karagwe wakimsikiliza mkuu wa wilaya wakati akitoa ratiba ya mbio za mwenge wilayani hapa. Picha na Shabani Ngarama

Laiser amesema maandalizi ya mapokezi ya mwenge yamekamiliks na kwamba kutakuwa na mikesha miwili kuanzia Septemba 3 na kisha uwanja katika stendi ya mabasi Kayanga Septemba 4. 2026 baada ya mwenge huo kukimbizwa umbali wa Km 50.5 kuanzia eneo la mapokezi

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Karagwe Julius Laiser