Karagwe FM

Dc Kyerwa ahimiza usafi kuepuka madhara ya mvua za el nino

12 October 2026, 13:24

Dc Zaituni Msofe akizungumza na wananchi wa Kyerwa baada ya usafi wa mazingira . Picha David Geofrey

Usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya ya jamii,kuzuia magonjwa ya mlipuko na kuimarisha ustawi wa uchumi na maumbile ya asili

Na: Mwandishi wetu

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Zaitun Msofe aongoza zoezi la usafi wa mazingira na kuwatolea wito wananchi wilayani Kyerwa kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu sanjari na kuchukua tahadhali dhidi ya mvua za el nino

Zoezi hilo lililofanyika katika maeneo ya Rwenkorongo yalipo makao makuu ya wilaya ya Kyerwa limewashirikisha wakazi wa maeneo hayo, watumishi wa umma, vyombo vya ulinzi na usalama , viongozi wa chama cha mapinduzi CCM, na viongozi wa kiroho.

Akihutubia washiriki baada ya zoezi hilo Msofe amewashukuru kwa kujitokeza kwa wingi na kutoa maelekezo kuhusu usafi ikiwa ni pamoja na kutoa tahadhari kuhusu mvua za el nino zinazotarajiwa hivi karibuni

Sauti ya Dc Kyerwa Zaituni Msofe