Sibuka FM

Programu ya Takukuru  Rafiki  kuondoa  Mianya  ya  Rushwa  Simiyu.

February 10, 2023, 10:15 am

Taasisi ya  kuzuia  na  Kupambana  na  Rushwa -TAKUKURU Mkoani  Simiyu  imeanza kutekeleza kampeni  ya  Takukuru  Rafiki lengo kupunguza na  kuzuia vitendo vya rushwa katika  ngazi ya kata na Vijiji.

Akitoa Elimu  hiyo  kwa Jamii kupitia Sibuka  fm Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Simiyu    Bi.  Janeth  Machulya  amesema tayari programu hii ya Takukuru  Rafiki imeanza kutekelezwa kwa kuanza  vikao katika ngazi ya kata vikihusisha  Madiwani na watendaji  wa Kata.

Bi Janeth  amesema Programu  hiyo ina Mazingira rafiki zaidi kwa Mwananchi bila kujali kuwa viongozi watakuwa miongoni mwao, jambo ambalo linaweza kuleta hofu kwa wananchi kutoa kero zao  na taarifa  zao  zitakuwa  Siri..

Sauti ya Bi Janeth Machulya- Mkuu wa Takukuru Simiyu

Hapa chini Picha za Matukio

Bi Janeth Machulya