Sibuka FM

Waziri Mashimba Ndaki akabidhi Komputa kwa shule za Sekondari jimboni kwake.

16 September 2021, 4:02 pm

Waziri  wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amewataka Wakuu wote wa shule za sekondari katika jimbo la Maswa Magharibi Mkoani  Simiyu kuanzisha madarasa ya kompyuta ili wanafunzi  kupata  maarifa  zaidi.

Waziri  Ndaki ambaye pia ni Mbunge wa jimbo hilo amesema hayo wakati akikabidhi kompyuta 10 na printa 2 kwa shule ya sekondari Buchambi na  shule ya sekondari Badi zilizoko wilayani hapa  ambapo kila shule ilipata kompyuta 5 na printa moja.

Sauti Waziri Mashimba Ndaki

     

Amesema kuwa  lengo la serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu  ni kuhakikisha inawajengea uwezo wanafunzi wa shule za sekondari kwa ajili ya somo la tehama ili kuendana na kasi na mabadiliko ya kiteknolojia.

Aidha amewataka walimu wa shule hizo ambazo wamekabidhiwa vifaa hivyo kuvitunza na kuhakikisha viko salama ili viweze kuwanufaisha wanafunzi katika masomo yao.

Sauti Waziri Mashimba Ndaki

      

Vifaa  hivyo vilivyokabidhiwa vyenye thamani ya sh Milioni 23.1 vimetolewa  na serikali kupitia mfuko wa mawasilino kwa wote  vitakuwa  ni  mkombozi  kwa walimu pamoja  na wanafunzi katika kusaidia suala zima la teknolojia pamoja na mawasiliano.