Sibuka FM

Maswa: Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa awataka watumishi wa serikali kutumia siku nne za kazi kuwahudumia wananchi wa vijijini

26 March 2023, 7:20 pm

Kwenye picha ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akihutubia wananchi walijitokeza katika ufunguzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hpspital ya wilaya ya Maswa hii leo 26.03.2023 .

Na Alex.F.Sayi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya kutumia siku nne za kazi kuwahudumia wananchi hasa wa Vijijini na sio kukaa maofisini wakisubiria ziara za viongozi wa juu kuwatembelea Wananchi.

Hayo ameyasema akiwa Ziarani Wilayani Maswa ,alipokuwa akizindua  Jengo la wagonjwa wa Dharura katika Hospitali ya Wilaya Maswa lililo gharimu  tsh,(mil 300)na mashine za matibabu kwenye Jengo hilo zenye thamani ya tsh,(mil,405)

“Nimeshazungumza na watumishi na tayari tumeshakubariana sasa wawatumikie wananchi kwa kasi kubwa zaidi na nimewaelekeza watumie siku(4)kwa siku za kazi kwenda kuwahudumia wananchi Vijijini hii itapunguza malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao,Serikali inaleta mabilioni ya fedha kama mnavyoona kama hamtawaeleza hawawezi kujua Serikali inafanya nini,Mama Samia anatoa fedha nyingi kwa ajili ya Miradi mbalimbali tunataka iwahudumie wananchi.Amesema Majaliwa.

Mhe.Majaliwa pia alitembelea kiwanda cha kuzalisha Chaki kilichopo maeneo ya Ng’hami Wilayani  hapa kilichojengwa kwa gharama ya tsh,(Bil 8)huku kiwanda hicho kikiwa kimekamilika kwa asilimia (100%)kikisubiria kuanza uzarishaji,ambapo kitakuwa na wafanyakazi zaidi ya (250)huku kiwanda hicho kikitarajiwa kuhudumia Mkoa wa Simiyu kwa kuzalisha katoni (120)kwa saa 16.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki,Mhe.Stanslaus Nyongo akizungumzia manufaa ya Jengo  la wagonjwa wa  dharura amesema  kuwa Jengo hilo litaweza kuwahudumia  wakazi  wa Wilaya ya Maswa na Wilaya Jirani kwa kuwa Jengo hilo  lipo kwenye njia kuu inayounganisha Wilaya zote za Mkoa wa Simiyu.

“Tunamshukuru Dkt. Samia kwa kutupa fedha kukamirisha ujenzi wa Jengo hili la Dharura hapa Maswa kwa kuwa hapa ni eneo sahihi  maana hapa Maswa ni njia kuu inayolisha Wilaya zote kwa Mkoa huu.”Amesema Nyongo.

Nyongo ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa imepokea zaidi ya tsh,(Bil 30)kwa Mwaka huu wa fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ikiwemo, Afya,Maji na Barabara ambapo kwa upande wa Afya tumejenga vituo vya Afya (6)natunaendelea na ukarabati wa zahanati, Theater(2)ya Mama Samia ya kisasa kabisa,(ICU) ya Watoto wadogo na Watoto Njiti yenye vifaa vya  kutosha kuliko Hospitali nyingine hapa Tanzania,Vifaa vya kisasa kabisa ikiwemo Mobile Xray na  Digital Xray mashine kubwa ambayo bado haijafungwa kwa kuwa hakuna Jengo lakuweza kufunga mashine hiyo.

“Mhe.Waziri uboreshaji huu wa huduma za Afya Wilayani Maswa umechangia  upungufu wa watumishi wa Afya,nikweli tunaishukuru Serikali tulipokea mgao wa watumishi wa Afya (46)lakini kutokana na maboresho na ujenzi wa vituo  vya Afya na Zahanati Wilayani hapa watumishi hawa sasa hawatoshi hivyo tunaiomba Serikali itusaidie watumishi.Amesema Nyongo.

“Mkoa umepokea zaidi ya tsh,(Bill 5)kwa ajili ya mradi wa Maji wa Ziwa.Victoria na sisi Maswa niwanufaika tunachoomba tu Mradi huo usitekelezwe kwa awamu ili wanamaswa tuweze kupata huduma hiyo kwa haraka zaidi,kwa kuwa Maswa bado inashida ya Maji,ingawa tunaishukuru Serikali kwa kutupatia tsh,(Bil 3.2) kwa ajili ya ununuzi wa Pump mpya na ujenzi wa Chujio kwenye chanzo chetu kikuu cha Maji Bwala la New Sola,na tumepata fedha tsh,Mil (400)kwa ajili ya kutandaza Bomba za kusambaza Maji kwenye Mji wa Maswa, tumejenga Tank la ujazo wa Lita Million moja lenye zaidi ya tsh,(Mil 497.3” Amesema Nyongo.

Aidha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Dr,Festo Dugange akitolea ufafanuzi utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Mkoani hapa amesema kuwa,Jengo hilo la wagonjwa wa Dharura ni kati ya majengo (80)yaliyojengwa Nchi nzima,na Mkoa wa Simiyu yamejengwa Majengo matatu Bariadi Vijijini,Wilaya ya Itilima na Meatu.

“Mhe.Waziri kwanza tunakushukuru sana kwa kukubali kulizindua Jengo hili maana litakuwa mkombozi kwa wakazi wa Wilaya hii,na Wilaya jirani kwani hapo awali wananchi walilazimika kwenda,Somanda Bariadi Mjini  ama Mwanza kupata huduma hii,kwa upande wa watumishi wa Afya ni kweli kabisa kama walivyo sema wabunge kunaupungufu wa watumishi, lakini Serikali inaendelea kulifanyia kazi na kwa Mkoa huu walipokea mgao wa watumishi wa Afya(227)na Wilaya ya Maswa ilipokea Mgao wa watumishi(62)na watumishi(12)wapo hapa Hospitali ya Maswa.”Amesema Dugange.