Sibuka FM

TRA YATOA ELIMU KWA WAFANYA BIASHARA WILAYANI MASWA JUU YA ULIPAJI KODI KWA HIARI.

16 September 2022, 11:10 am

Mkuu  wa  Wilaya  ya Maswa  Mkoani  Simiyu  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa   Wananchi  wanatakiwa  kuwa  Wazalendo  kwa  Kulipa  Kodi  ya Serikali kwa  Maendeleo  ya  Taifa.

Mh  Kaminyoge  ametoa  wito  huo  kwenye  kikao kati  ya  Wafanyabiashara wilayani  hapo   na  Maafisa  wa  Mamlaka  ya  Mapato  TRA    chenye  lengo  la Kujadili  Mabadiliko  ya  Kodi  kulingana  na  Sheria  ya  Fedha  ya  Mwaka 2022.

“Nipende tu kusema kwamba   Serikali  haifanyi Biashara, Serikali inakusaya Kodi  kwa  ajili ya  kazi  hizo, sasa jambo  kubwa  kwa  wananchi  ni  kulipa  Kodi  na  Serikali inarudisha  Kodi  hizo kwa ajili ya  Maendeleo.

Ndio maana  TRA  wamekuja  Kuelimisha ili  Sote  kwa  pamoja tuede katika  Mstari  mmoja,Kazi  yangu  kubwa  kama  mkuu wa Wilaya  ni kuhakikisha  Usalama, Amani  na  Utulivu  ili nyinyi kufanya kazi  pasipo matatizo  yoyote”

Mkuu  wa  Wilaya  huyo  Amesema  kuwa   Mwaka  wa  Fedha  2021/2022  Wilaya  ya Maswa  ilipokea Fedha  nyingi  kwa  ajili  ya  Miradi mbalimbali  ya  Maendeleo  hivyo  Kodi  wanayotozwa  Wananchi  ndio  inayorudi  kwa  ajili  ya  maendeleo..

“Upande  wa  Afya Mh  Rais   ameleta  Fedha nyingi  sana  kwa  ajili  ya  Wananchi  wake, Katika  kipindi  kifupi  cha  Mwaka  mmoja Tumejenga vituo  vya Afya  zaidi  ya Vitano  nyie  wafanyabiashara  ni Mashahidi  maana  hata  vifaa vya  Ujenzi  baadhi  tumenunua  kwenye Maduka  yenu.

Leo  hii  serikali   sisi  watu  wa  Maswa  Imetuheshimisha  imesema  itatutengenezea Barabara  ya  kutoka Maswa kupitia Lalago, Meatu, Sibiti, Haidom  hadi  Karatu  mkoani  Arusha  kwa  Kiwango  cha  Lami  sasa  ni masaa matatu au manne kwenda  Arusha  hapo  hatujataua  Mji, hatujafanya  Biashara”

Joseph  Mtandika  ni  Meneja  Mamlaka  ya  Mapato- TRA    Mkoa   wa  Simiyu  amewapongeza  Wananchi  wa  Mkoa  wa  Simiyu  kwa  Kuvuka  lengo  la  Ukusanyaji  wa  Mapato  kwa  Mwaka  wa  Fedha  2021/2022  huku  Wilaya  ya  Maswa  ikfikia  Asilimia  92%   ya  Makusanyo  yote..

“Niwashuru sana Wana  Maswa  Mwaka  Jana katika Malengo tulikuwa Tukusanye milioni 717  lakini  tukaishia  kukusanya Asilimia  92, lakini  mwaka  huu  lengo  limeongezeka  tunatakiwa  tukusanye  Milioni 940.3  pamoja na  mabadiliko  ya  sheria ya  Fedha   ndio maana  tumekuja  hapa kuwakumbusha  wajibu  wenu wa  kulipa  Kodi  kwa  Hiari  bila  kufukuzana bila  kukimbizana ili tuweze  kufikia  Lengo letu la Milioni 940.3”

Akifungua  Kikao  hicho  Kaimu  Mwenyekiti wa  Wafanya biashara  Wilaya  ya  Maswa   Emmanuel  Mlyazenze   amesema  kuwa  Elimu  waliyoipata  iwasaidie  kuwa  Waamifu  na  Wazalendo  katika  Ulipaji  wa  Kodi a  kuwa  Mabalozi  kwa  Wafanyabiashara  wenzao  ambao  hawakufanikiwa  kufika  kwenye  Kikao  hicho.

Baadhi ya  Wafanyabiashara  Walioshiriki  Kikao  hicho  Wameishukuru  TRA  kwa  Elimu  waliyowapatia   Juu  ya  Ulipaji  Kodi huku  akiwaomba  Maafisa  wa  TRA  kujenga Mahusiano  Mazuri  kwa  Wateja   wao  ili  kuleta  Ushawishi  wa Ulipaji  wa  Kodi  kwa  Hiari.

 

Hapa  chini  ni  picha  za  matukio mbalimbali ya Kikao cha  Wafanyabuiashara na  TRA  Wilaya  ya  Maswa.