TFS yahimiza kutunza mazingira kwa kupanda miti
9 December 2024, 8:19 pm
Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara kiwilaya Sengerema yamefanyika shule ya Msingi Lumeya katika halmashauri ya Buchosa ambapo miti 2000 imepandwa kama kumbukumbu ya maadhimisho hayo mwaka huu.
Na;Emmanuel Twimanye
Wakala wa Huduma za Mistu Tanzania (TFS) wilayani Sengerema mkoani Mwanza imewataka wananachi kutunza miti iliyopandwa ili kutunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Kauli hiyo imetolewa na Mhifadhi mkuu wa wakala wa huduma za mistu (TFS) Wilaya ya Sengerema Stephen Odongo Oyugi katika Sherehe ya miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara zilizo kwenda sambamba na zoezi la upandaji wa miche ya miti elfu mbili katika shule ya Msingi Lumeya Halmshauri ya Buchosa.
Katibu tawala wa wilaya ya Sengerema Curthbert Midala aliye mwakilisha mkuu wa wilaya ya Sengerema katika sherehe hiyo amesema kuwa wilaya hiyo imeadhimisha shehere hizo kwa kupanda miti katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lumeya Mwl.Msagaa kitikuhango ame wa ahidi kuitunza miti hiyo.
Nao baadhi ya wananchi walio hudhuria katika sherehe hizo wame ahidi kushirikiana kwapamoja na uongozi wa serikali ya kijiji na shule kulinda na kutunza miti iliyopandwa huku wakipongeza wakala wa huduma za mistu wilaya ya Sengerema kwa kutoa miche hiyo ya miti.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu wa kutimiza Miaka 63 ya uhuru wa Tanzania bara
Uongozi madhubuti na ushirikishwaji wa wananchi ni msingi wa maendeleo yetu