TYC Yaja na program ya kilimo sauti kwa vijana nchini
24 October 2024, 3:58 pm
Shirika la TYC limekuwa likijishughulisha na program mbalimbali za kuwasaidia vijana kuondoka na changamoto ya uhaba wa ajira nchini Tanzania kupitia kilimo.
Na;Deborah Maisa
Vijana nchini wametakiwa kujikita katika sekta ya kilimo ambayo inachangia kutoa nafasi za ajira kwa kiaasi kikubwa nchini.
Rai hiyo imetolewa na meneja mradi kutoka shirika la Tanzania youth coalition anayesimamia kilimo sauti katika wiki ya vijina mkoa wa Mwanza ambapo amesema kwa sasa sekta ya kilimo imekuwa ikihudumia takribani maeneo mengi hivyo vijana wajikita katika kilimo biashara.
Nae afisa mradi wa boresha maisha ya vijana amesema kkuwa katika wiki ya vijana mradi wa boresha maisha ya vijana wamewawezesh baadhi ya vijana kutoka katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma,naIringa,na wameendelea kunuafaka kupitia miradi huo.
Kwa upande wao wanufaika wa miradi hiyo wamelishukuru shirika la TYC kwakuwawezesha kuwakutanisha na vijana mbalimbali katika wiki ya vijana mkoa wa mwanza.
Wiki ya vijana kitaifa imefanyika mkoni Mwanza na kuambatana na kumbukumba ya baba wa taifa nwalimu Julius kambarage nyerere pamoja na uzimwaji wa mwenge wa uhuru.