Sengerema FM

Sengerema yapanda miti elfu 5 sikukuu ya kuzaliwa Rais Dkt. Samia

27 January 2026, 10:57 pm

Mkuu wa wilaya ya Sengerema na baadhi ya wananchi na wanafunzi wakiwa kwenye picha ya pamoja zoezi la upandaji miti.Picha na Elisha Magege

Wilaya ya Sengerema imeungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano kusherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kupanda miti zaidi ya elf 5, huku ikiwahimiza wananchi kujenga utamaduni wa kupanda miti.

Na;Elisha Magege

Katika kuazimisha siku ya kuzaliwa kwa rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. Samia Suruhu Hassan wilaya ya Sengerema imepanda Zaidi ya miti elf 5 kwenye tasisi mbalimbali za kijamii.

Akiongoza zoezi hilo mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga amesema wameitumia siku hii kuungana na Rais Dr. Samia kupanda miti kama anavyo himiza jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi. Senyi Ngaga

Kwa upande wake mhifadhi mkuu TFS Wilaya ya Sengerema Steven Odongo oyungi ameendelea kuwahimiza wananchi kupanda miti kwani mamlaka hiyo inaotesha miche na kuigawa bure kwa wananchi.

Sauti ya mhifadhi mkuu TFS Wilaya ya Sengerema Steven Odongo oyungi

Naye askari Mhifadhi TFS wilaya ya Sengerema Samwel Magina ameishukuru jamii kujitokeza kupanda miti, kwani suala hilo linamanufaa kwa jamii yote kwa ujumla.

Sauti ya askari Mhifadhi TFS wilaya ya Sengerema Samwel Magina

Kampeni ya 27 ya Kijani inayohamasisha kupanda miti, kama njia ya kutunza mazingira inaendelea, sambamba na kumbukizi ya kuzaliwa kwa rais Dr. Samia Suruhu Hassani tar 27 January 1960, na mwaka huu ametimiza miaka 66 .