Sengerema FM
Sengerema FM
20 January 2026, 7:25 pm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani ametoa eneo la hifadhi la ukubwa wa hekali 1200 kwa wananchi wa vijiji vya Ihushi na Bujura miyenze,na kusisitiza kuwa na hati za kimila.
Na,Said Mahera
Wananchi wa Kijiji cha Ihushi Kata ya Shabaka wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita wametakiwa kuchangamkia fursa ya kumiliki ardhi kwa kupata hati miliki za kimila.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa halimashauri ya wilaya ya Nyang’hwale, Ndg. Husna Toni katika Mkutano wa kuhamasisha Wananchi juu ya kujitokeza kwenye mchakato wa kupatiwa hati miliki kwani zitawasaidia Wananchi kuwa na uhakika wa kumiliki ardhi yao bila kuwa na migogoro usumbufu wa aina yoyote.
Amesema, Ofisi ya Tume ya Taifa ya Mipango na Matumizi bora ya Ardhi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji inaendesha zoezi hilo la kuwapatia Wananchi hati miliki za kimila kwenye ardhi wanayoimiliki.
Nae Bwn Slyvanus Cosmas diwani wa kata ya Shabaka, amemshukuru Mh Rais Samia kwa kuwapatia hekari 331 katika kata yake ambazo zitakwenda kuwanufaisha wananchi wa kata hiyo ambao hawakuwa na maeneo ya makazi pamoja na kuwasaidia wafungaji.
Kwa upande wao Wananchi wa Kijiji cha Ihushi wamemshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kuwapatia ardhi hiyo itakayowasaidia kwa ajili ya makazi, kilimo, ufugaji na shughuli nyengine.
Zoezi la ugawaji wa hati za kimila 1,200 limekuja baada ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuridhia kugawa eneo la hifadhi kwa vijiji viwili kijiji cha Ihushi kpamoja na kijiji cha Bujura Miyenze kata ya mingilo
