Sengerema FM
Sengerema FM
10 June 2025, 6:14 pm

Kufuatia uwepo wa matukio ya uvunjifu wa amani kuelekea uchaguzi mkuu 2025 viongozi na wamini wa kanisa la Baptist Sengerema wameungana na kufanya maombi ya kuliombea taifa ili liendelee kuwa kisiwa cha amani kama inavyotambulika kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani.
Na,Joyce Rollingstone
Umoja wa Makanisa ya Baptist Wilayani Sengerema wamefanya maombi maalum kwa ajili ya kuombea Amani Taifa la Tanzania, katika kuelekea uchaguzi Mkuu Octobar Mwaka huu.
Maombi hayo yamefanyika katika kanisa la Baptist ishingisha lililopo katika kata ya Sima Wilayani Sengerema,ambapo mshauli wa makanisa ya Baptist askofu mstaafu wa kanda ya ziwa Boniphas.K. Mponeja wa kanisa la Baptist Gethsemane Igogo A,amewaomba waumini wote kuilinda Amani iliyopo.
Aidha waumini walioshiriki maombi hayo,wameahidi kuwa watailinda na kuidumisha Amani iliyopo kwani ikipotea ni vigumu kuilejesha.
Sambamba na hayo,pia umoja huo umejumuisha upokeaji wa fedha za ujenzi wa kanisa la Baptist Igogo A,ununuzi wa kiwanja cha kanisa,pamoja na ununuzi wa vyombo vya kwaya,ambapo mwakilishi wa aliyekuwa mbunge wa jimbo la Sengerema Mh Wiliamu Mganga Ngeleja, Ndug,Lugega Festo Petro,amekabidhi fedha hizo ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyokuwa imetolewa huku akiwataka kuendelea kuilinda Amani iliyopo.
Naye asikofu wa makanisa ya Baptist sengerema Eliasi Kusaya, ameshukuru aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sengerema Dkt.Willium Mganga Ngereja kwa kuunga mkono juhudi za neon la Mungu.
Hata hivyo, maombi hayo yamehudhuliwa na viongozi mbalimbali wa makanisa ya Baptis, pamaja na waumini .