Sengerema FM
Sengerema FM
21 May 2025, 7:10 pm

Mei 20 2025 nchini Tanzania ilienea taarifa ya udukuzi kwenye mitandao ya kijamii ya baadhi ya tasisi za kiserikali na za watu binafsi,jambo lililowaimbua wataalamu wa mitandao nchini kuitaka jamii ya watanzania kuwa makini na mitandao hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu 2025.
Na.Elisha Magege
Jamii imetakiwa kuwa makini na taarifa zinazo chapishwa kwenye mitandao ya kijamii kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Rai hiyo imetolewa na Mwita Mroni mtaalamu wa ulinzi mtandaoni katika kipindi cha ukurasa wa vijana cha Radio Sengerema, ambapo amesema kuelekea kipindi cha uchaguzi taarifa nyingi za uongo huchapishwa sambamba na matukio ya udukuzi hufanyika kwa maslahi ya watu wabaya.
Nao baadhi ya wananchi mjini Sengerema wamesema kuenea kwa taarifa za uongo kupitia mitandao ya kijamii inaweza kusababisha machafuka katika nchi.
Katika kukabiliana na changamoto za udukuzi na kuzangaa kwa taarifa za uongo mtandaoni kituo cha habari na mawasiliano Sengerema Telecentre kimeandaa program maalumu itakayo fundishwa kwa jamii ili kujua namna ya kujilinda na kufahamu taarifa za uongo.
Mapema may 20 2025 kuna taarifa zilienea nchini zikionesha udukuzi na kuchapishwa kwa taarifa za uongo kwenye baadhi ya mitandao maalumu ya kiserikali na watu maarufu nchini Tanzania, jambo lililomlazimu msemaji mkuu wa Serkali Bwn. Gersoni msigwa kutoa ufafanuzi juu taarifa.
