

21 March 2025, 7:31 pm
Kila mwaka Machi 22 huwa ni Siku ya Maji ambayo huadhimishwa kimataifa kutokana na na Azimio Na. 47/193 la Umoja wa Mataifa (UN), ambapo Wakala wa Maji Vijijini RUWASA wialayani Sengerema umetoa msaada kwa wafungwa na kupanda miti kwenye vyanzo vya maji.
Na,Emmanuel Twimanye
Wakala wa Maji vijijini (RUWASA) wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo taulo za kike kwa wafungwa na mahabusu katika gereza la Kasungamile .
Akikabidhi msaada huo kwa viongozi wa Gereza hilo kaimu Meneja wa wakala wa maji vijiiini Wilayani Sengerema Tyson Magagala amesema kuwa wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya maji Duniani.
Kaimu mkuu wa Gereza la Kasungamile amewashukuru wakala wa maji kwa kutoa msaada huo kwani utawasaidia wafungwa na mahabusu .
Katika hatua nyingine wakala wa maji wametumia sehemu ya maadhimisho hayo ya wiki ya maji kwa kupanda miti mia tano katika chanzo cha maji Katwe Halmshauri ya Buchosa ili kuitunza mazingira.
Nao baadhi ya wananachi wa Katwe wamepongeza Ruwasa kwa kupanda miti hiyo huku wakiahidi kuitunza .