Sengerema FM

Dawa za kienyeji bila vipimo zatajwa kuwa hatari kwa figo

15 March 2025, 1:59 pm

Picha ikionyesha figo yenye changamoto na nyingine ikiwa salama.Picha na wizara ya afya

Kila Alhamis ya pili ya mwezi Machi Dunia huadhimisha Siku ya Figo ikiwa na lengo la kutoa elimu ya namna bora ya kutunza na kuepukana na magonjwa yanayoweza kuleta madhara makubwa kwa figo.

Na John Sospiter.

Wananchi wilayani Sengerema mkoani Mwanza wametoa maoni yao juu ya siku ya figo duniani ambayo huadhimishwa kila Alhamisi ya pili ya mwezi wa tatu ambapo kwa mwaka huu imeadhimishwa Machi 13, 2025.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na redio Sengerema Yasinta Machenga pamoja na Renatus Faustine wamesema kuwa siku ya figo duniani ipo kwa ajili ya kuikumbusha jamii na kupata elimu juu ya magonjwa yanayoweza kuathiri figo.

Sauti za wananchi mjini Sengerema wakizungumzia ugonjwa wa figo

Naye Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Sengerema Dkt. Godfrey Silayo amesema kuwa magonjwa ya figo husababishwa na vitu tofauti tofauti kama vile shinikizo la damu, kisukari, mzio, magonjwa ya kurithi ambayo yanaweza kuathiri figo na kuongeza kuwa matumizi ya miti shamba bila kipimo huweza kusababisha kuharibu figo.

Sauti ya Mganga mfawidhi wa kituo cha afya Sengerema Dkt Godfrey Silayo akizungumzia vyanzo vya magonjwa ya figo.

Hata hivyo kulingana na takwimu za wizara ya afya imeonyesha kuwa asilimia 7 ya watanzania wanaishi na ugonjwa wa figo ambapo takwimu Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), vifo vinavyotokana na magonjwa ya figo duniani kote vinakadiriwa kuwa kati ya milioni 5 hadi11 kila mwaka, na mara nyingi huathiri nchi zenye kipato cha chini na cha kati.