Sengerema FM

Zaidi ya mil.300 kutolewa mikopo ya 10% Sengerema

1 March 2025, 6:44 pm

Bi. Jospina Bryson akitoa maelekezo kwaa wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi Sengerema. Picha na Elisha Magege

Wananchi wameonyesha kufurahia baada ya mikopo ya asilimia kumi kurejeshwa huku wakidai wameumizwa sana na kausha damu baada ya serkali kusitisha mikopo hiyo kwa vijana,wanawake na wenye ulemavu.

Na,Elisha Magege

Halmashauri ya Sengerema imetoa mafunzo ya siku moja ya namna bora ya usimamizi wa miradi ya ujasiriamali kwa vikundi vilivyoomba mikopo ya asilimia 10.

Akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Mkuu wa idara ya Mazingira Ally Salim ameviasa vikundi vinavyo talajia kupata mikopo, kuzingati mafunzo hayo ili badae viweze kutekeleza vyema miradi yao na badae kurejesha mikopo kwa wakati ili kuwezesha vikundi vingine kunufaika na mikopo hiyo.

Sauti ya Kaimu mkurugenzi Halmashauri ya Sengeerema Ally Salim

Bi. Jospina Bryson akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii halmashauri ya Senngerema, amesema lengo la mafunzo hayo ni kuviwezesha vikundi vilivyokidhi vigezo ili viweze kutekeleza vyema miradi mbalimbali ya ujasiliamali  ambapo amesema kwa awamu hii Halmashauri itatoa mikopo ya shilingi mlioni 362 kwa vikundi 111.

Sauti ya Bi. Jospina Bryson mratibu wa mikopo ya asilimia kumi Halmashauri ya Sengerema

Nao baadhi viongozi wa vikundi wanaotarajiwa kunufaika na mikopo hiyo wameushukuru uongozi wa Halmashauri ya Sengerema kwa kuwapatia mafunzo hayo ambapo wamesema yatasaidia kuboresha miradi yao kama vile ufugaji wa kisasa pamoja na kufanya biashara kwa kuzingatia wakati uliopo.

Sauti zza wanufaika wa mikopo ya Asilimia 10 wilayani Sengerema

Mafunzo yaliyotolewa kwa vikundi hivyo ambapo ni   vikundi vya wanawake 82, vijana 18 na  wenye ulemavu vikundi 11 ni kuhusu Kilimo Biashara, Ufugaji wa kisasa, Utunzaji wa mazingira pamoja na biashara.