

19 February 2025, 1:04 pm
Halmashauri ya Sengerema inapatikana katika mkoa wa Mwanza ambapo ni lango kuu la watu kutoka mikoa ya kagera, kigoma, Geita na nchi jilani kuingia katika jiji la Mwanza,hivyo inatajwa kuwa sehemu iliyo kwenye hatari kubwa ya kukumbwa na ugonjwa marburg.
Na,Elisha Magege
Wahudumu wa afya ngazi ya jamii Halmashauri ya Sengerema wameendelea kupewa mafunzo ya kukabiliana na ugonjwa wa homa ya Marburg uliotajwa kuibuka katika Wilaya ya Bihalamalo mkoani Kagera.
Wakizungumza baada ya mafunzo hayo, wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wao na kutoa elimu hii kabla ya ugonjwa huo haujaeneo kwa kasi kwenye maeneo yao na kwamba wataendelea kuielimisha jamii ili ijikinge na maabukizi ya Marburg.
Kwa upande wake Dr. Abdurahman Mgonja Mratibu wa Magonjwa ya mulipo Halmashauri ya Sengerema amesema mafunzo hayo kwa wahudumu wa afya ngazi ya Jamii yanalenga kuimalisha mfumo wa utoaji elimu kwa umma kuhusu magonjwa ya mulipuko yanayotokea nchini.
Licha ya kutokulipotiwa kisa cha ugonjwa huo katika Halmasahuri ya Sengerema, ugongonjwa huo umeripotiwa katika Wilaya ya Bihalamulo mkoani Kagera ambapo kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya hospitali ya Rufaa ya mkoa Bukoba ikimunukuu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt.Ntuli Kapologwe inasema watu 2 wamefariki dunia kwa Marburg na wahisiwa 15 wamewekwa karantini na wengine 281 waliochangamana na wahisiwa hao wakiendelea kusakwa.