Baraza la Madiwani Sengerema lapitisha Bajeti ya Bilioni 66
19 January 2025, 2:30 pm
Halmashauri ya Sengerema kwa bajeti ya Mwaka 2023/24 iliweza kufanya vizuri na kuvuka lengo kwa Asilimia 115 na bajeti ya sasa ya 2024/25 mpaka kufikia january hii imefikia asilimia 55,pia imepitisha mpango wa bajeti wa 2025/26.
Na;Elisha Magege
Halmashauri ya Sengerema imepitisha mpango wa bajeti ya Tsh.Bil.66 kwa mwaka wa fedha 2025/26 huku ikitaja vipaumbele ni ujenzi wa soko na Stendi mpya bukala.
Akizungumza baada ya madiwani kupitisha mpango wa bajeti hiyo Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya Sengerema Binuru Mussa Shekidele amesema Bajeti hiyo imezingatia vipaumbele vyote vinavyohitajika kwa wananchi wa Sengerema ikiwemo uboreshaji na ujenzi wa stendi mpya Bukala na soko kuu mjini Sengerema.
Nao madiwani wa Halmashauri ya Sengerema wamesema mpango wa bajeti hiyo ikifanikiwa itasaidia wananchi kunufaika na miradi iliyopo kwenye bajeti hiyo.
Aidha baadhi ya wafanya biashara soko kuu mjini Sengerema wamesema edapo bajeti hiyo itapitishwa basi ujenzi wa soko utasaidia wao kuongeza kipato na kusongeza huduma kwa wananchi.
Makadilio ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/26 ni mapato ya ndani ni Tsh bil.3.3, Ruzuku na mishahara Bil.Tsh bil.44.2, Matumizi mengineyo ni Tsh.Bil.1.4 Na miradi ya maendeleo ni Tsh. Bil 17.3 Ambapo jumla kuu ni Tsh.Bilion 66.3