Mke amtelekezea watoto wanne mme wake baada ya kupofuka
26 October 2024, 9:00 am
Changamoto ya wanawake kuishi na waume zao wanapopata changamoto za kidunia imekuwa ikishamili kwa maeneo mengi nchini, ambapo mala nyingi wamekuwa wakidai hawawezi kamwe kuishi na wanaume wasio na uwezo wa kutafta pesa.
Na;Emmanuel Twimanye
Mwanamke mmoja katika Kijiji cha Nyamililo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza amedaiwa kutelekeza watoto wake wanne baada ya mme wake kupata ulemavu wa macho.
Akizungumzia kisa hicho Baba wa familia hiyo Mussa Ramadhani amesema kuwa baada ya kupata ulemavu wa macho ndipo mke wake akawatelekeza watoto na kutokomea kusikojulikana hali inayomlazimu kuishi katika maisha magumu na watoto ikiwemo kulala njaa kwa kukosa chakula huku akiwaomba wasamalia wema kumsaidia kwa chochote.
Mtoto Junior Mussa Ramadhani anayemtembeza Baba yake mjini Sengerema kwa ajili ya kuomba msada kwa wasamalia wema ili wapate chakula ameiomba serikali kuwasaidia mtaji ili wafanye biashara itakayowawezesha kuendesha familia .
Baadhi ya wananachi wamesikitishwa na kitendo cha mwanamke kutelekeza familia baada ya mme wake kupata ulemavu wa macho na kuwaomba wanawake kuwa wavumilivu katika ndoa zao .
Naye mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Wilayani Sengerema Mponela Malongo ameahidi kuisaidia familia hiyo huku akiwaomba wanawake kuwa wavumilivu katika ndoa zao katika nyakati za shida na raha.