Sengerema FM

TYC Yaja na program ya kilimo sauti kwa vijana nchini

24 October 2024, 3:58 pm

Edward Lalika afisa mradi wa boresha maisha ya vijana akizungumza na wateja waliofika kwenye banda la shirika la TYC. Picha na Deborah Maisa

Shirika la TYC limekuwa likijishughulisha na program mbalimbali za kuwasaidia vijana kuondoka na changamoto ya uhaba wa ajira nchini Tanzania kupitia kilimo.

Na;Deborah Maisa

Vijana nchini wametakiwa kujikita katika sekta ya kilimo ambayo inachangia kutoa nafasi za ajira kwa kiaasi kikubwa nchini.

Rai hiyo imetolewa na meneja mradi kutoka  shirika la Tanzania youth coalition anayesimamia kilimo sauti katika wiki ya vijina  mkoa wa Mwanza ambapo amesema kwa sasa sekta ya kilimo imekuwa ikihudumia takribani maeneo mengi hivyo vijana wajikita katika kilimo biashara.

Sauti Ernest Seko meneja mradi kutoka  shirika la Tanzania youth coalition akizungumzia program ya kilimo sauti

Nae afisa mradi wa boresha maisha ya vijana amesema kkuwa katika wiki ya vijana mradi wa boresha maisha ya vijana wamewawezesh baadhi ya vijana kutoka katika mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dodoma,naIringa,na wameendelea kunuafaka kupitia miradi huo.

Sauti ya Edward Lalika afisa mradi wa boresha maisha ya vijana akizungumzia namna vijana wanavyonufaika na miradi kilimo sauti

Kwa upande wao wanufaika wa miradi hiyo wamelishukuru shirika la TYC kwakuwawezesha kuwakutanisha na vijana mbalimbali katika wiki ya vijana mkoa wa mwanza.

Sauti za wanufaika wa mradi wa kilimo sauti

Wiki ya vijana kitaifa imefanyika mkoni Mwanza na kuambatana na kumbukumba ya baba wa taifa nwalimu Julius kambarage nyerere pamoja na uzimwaji wa mwenge wa uhuru.