Diwani apongeza maboresho miundombinu ya elimu Mayuya
24 September 2024, 8:33 pm
Shule ya msingi Mayuya ni miongoni mwa shule zilizokuwa zikifanya vibaya kwenye mitihani yake kutokana na uhaba wa vitendea kazi kwa walimu pamoja na miundombinu iliyokuwepo kuchakaa, jambo lililomlazimu diwani wa kata hiyo kuchukua hatua ya kuanza kuboresha miundombinu ya walimu kwa lengo la kuinua ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.
Na;Emmanuel Twimanye
Diwani wa kata ya Tabaruka Mh. Sospeter Busumnabu ameupongeza uongozi wa shule ya msingi Mayuya kwa kukarabati miundombinu ya shule pamoja na kutengeneza samani za ofisi za walimu zenye zaidi ya shilingi milioni moja kwa kutumia fedha za ukarabati na rasilimali za shule.
Pongezi hizo zimetolewa na Diwani huyo wakati akikabidhi samani hizo kwa uongozi wa shule hiyo kwa kuwa wa kwanza kukarabati miundombinu kati ya shule zote zilizopo katika kata ya Tabaruka ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa katika kikao cha maendeleo ya kata hiyo kwa shule zote kuhakikisha zinafanya hivyo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mayuya Bwn ,Ladislaus Zacharia pamoja na kupongeza hatua hiyo amewaomba walimu kuendelea kuwafudisha wanafunzi kwa bidii ili kuwasaidia wanafunzi kufikia ndoto zao na kupata viongozi watakaolisaidia Taifa hapo badae kutoka katika shule hiyo.
Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Mayuya Nkandala Kahemejo ameupongeza uongozi wa shule kwa kupiga hatua kubwa kwa kuboresha miundombunu .
Uongozi wa shule hiyo umeahidi kufanya mabadiliko makubwa Zaidi ikiwa ni pamoja na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi .
Nao baadhi ya walimu wameshukuru Diwani wa kata hiyo na Uongozi wa shule kwa kukarabati miundombiny hiyo kwa kuwa itawasaidia kufundisha katika mazingira rafiki .