Madaktari bingwa wa Rais Samia kuweka kambi ya siku tano Sengerema
13 June 2024, 2:13 pm
Kambi za matibabu ya madaktari bingwa wa Rais Samia katika hospitali za Halmashauri za wilaya zinasaidia kupunguza rufaa kwa wagonjwa kwenda katika hospitali za kanda na taifa pia kupelekea kupunguza gharama za matibabu kwa wananchi.
Na:Elisha Magege
Jamii imetakiwa kuchangamkia fulsa za uchunguzi na matibabu kutoka kwa madaktari bingwa wa Rais Samia wanao zunguka nchi nzima kutoa huduma za kibingwa na kibobezi kwa magonjwa mbalimbali.
Rai hiyo imetolewa na Dr. Christopher Benard Mganga mfawidhi Hospitali ya wilaya ya Sengerema alipokua akizungumza na Radio Sengerema kuhusu ujio wa madaktari hao bingwa halmashauri ya Sengerema.
Katika hatua nyingine Dr. Benard amesema kambi hiyo ya madaktari bingwa itakuwepo kwa siku nne kuanzia tar17-21 mwezi huu wa sita (6) na watafanya huduma mbalimbali za kitabibu kwa wananchi.
Huduma ya matibabu ya madaktari bingwa wa Rais Samia kwa mkoa wa Mwanza itatolewa katika maeneo ya Hospitali za wilaya ambapo kwa Sengerema huduma itatolewa katika Halmashauri ya Sengerema Hospitali ya Mwabaruhi na Halmashauri ya Buchosa Katika Hospitali ya wilaya Isaka.