Sengerema FM

Shirika la CLWF kutoka Korea laanza kujenga Madarasa Sengerema

18 May 2024, 7:42 pm

Picha ni Makamu wa  Rais wa shirika la CLWF Methew Lubongeja  akikagua ujenzi wa misingi ya vyumba vya madarasa shule ya Msingi Isole.Picha na Emmanuel Twimanye

Shule ya Msingi Isole iliyopo kata ya Buyagu Halmashauri ya Sengerema imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa muda mrefu, hali iliyopelekea shirika la CLWF kujitolea kujenga vyumba vinne vya madarasa shuleni hapo.

Mkurugenzi wa Shirika la CLWF Bwn. Joshua John wapili kushoto akipitia taarifa ya ujenzi wa madarasa hayo inayosomwa na viongozi wa kijiji cha Isole.

Na;Emmanuel Twimanye

Shirika lisilokuwa la kiserikali la Christian Life World Mission Frontiers kutoka nchini Korea Kusini  limeanzisha ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa katika shule ya Msingi Isole iliyopo Kata ya Buyagu Wilayani Sengerema ili kutatua  changamoto ya mlundikano wa wanafunzi Darasani .

Akizindua ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa  vinavyotarajia kugahrimu Zaidi ya shilingi milioni 40  Mkurugenzi wa shirika hilo nchini Tanzania Joshua John  amesema kuwa  wameamua kutoa msaada huo ili kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta ya elimu.

Sauti ya Mkurugenzi wa Shirika la CLWF Bwn. Joshua John

Makamu wa  Rais wa shirika hilo Methew Lubongeja  amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza  kusababisha kupata ujauzito na kukatisha ndoto zao za kielimu.

Sauti ya Makamu wa  Rais wa shirika la CLWF Methew Lubongeja 

Mwalimu mkuu  wa shule hiyo na baadhi ya viongozi  wa kata hiyo  pamoja na kushukuru shirika hilo kwa msaada huo wameahidi kusimamia ujenzi huo ili ukamilike  kwa wakati.

Sauti za Viongozi kijiji cha Isole Sengerema

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo  wamesema kuwa wamekuwa wanasoma wakiwa wamelundikana Darasani hivyo  utakapokamilika   ujenzi wa madarasa hayo itasaidia kusoma katika mazingira rafiki sambamba na kuongeza ufaulu.  

Sauti za Wanafunzi Shule ya Msingi Isole