Sengerema yakabidhi madarasa 129 ya uviko 19.
6 January 2022, 10:42 pm
Jumla ya vyumba vya madarasa mia moja na ishirini na tisa vilivyojengwa kwa fedha za uviko 19 halimashauri ya wilaya ya Sengerema vimekamilika na kukabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza tayali kusubilia wanafunzi kuanza masomo yao january17 mwaka huu.
Akikabidhi madarasa hayo mkuu wa wilaya ya Sengerema Bi.Senyi Ngaga amesema madarasa hayo yamekamilika kwa asilimia 98 kwa halmashauri ya Sengerema huku akimpongeza mh.Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajiri ya ujenzi wa madarasa na miradi mingine.
Kwa upande wao mbunge wa jimbo la Sengerema Mh.Hamis Tabasam na mwenyekiti wa halmashauri ya Sengerema Mh.Yanga Makaga kwa pamoja wamemshukuru rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za madarasa katika halmashauri hiyo.
Akipokea madarasa hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Ngussa Samike ambae pia ni katibu tawala mkoa wa Mwanza amewapongeza viongozi wa halmashauri ya Sengerema kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mpaka kufanikisha ujenzi wa madarasa yote yaliyojengwa kwa fedha zilizotolewa na rais Samia huku akiwaomba fedha zilizo baki zijenge matundu ya vyoo ilikuendana na wingi wa madarasa yaliyo jengwa.
Halmashauri ya Sengerema imepokea fedha jumla ya shilingi Bilion 2.8 kwa ajiri ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 129, ambapo mpaka sasa madarasa hayo yamekamilika pamoja na madawati yake huku ikibakiwa na salio la fedha na vifaa.