Orkonerei FM

Kichwa cha Habari: Faida za Mama Kujifungulia Hospitalini na Hatari za Wakunga wa Kienyeji Zabainishwa

17 March 2026, 10:01 am

Na Baraka Olemaika

Akina mama wajawazito nchini wameshauriwa kuhakikisha wanajifungulia katika vituo vya afya ili kupata huduma stahiki na kuokoa maisha yao na ya watoto wao, huku wakionwa dhidi ya hatari zinazoweza kujitokeza wanapojifungulia nyumbani.

Akizungumza katika mahojiano maalum, Anastazia Medadi, Muuguzi Mkunga kutoka Zahanati ya Terat, amebainisha kuwa huduma za kitaalamu wakati wa uchungu na uzazi ni muhimu katika kuzuia vifo visivyo vya lazima.

Anastasia ametoa wito kwa wakunga wa jadi kushirikiana na serikali kwa kuwaleta wajawazito hospitalini badala ya kuwazalisha majumbani.

“Ushauri wangu ni kwamba mama anapoanza kuhisi dalili za uchungu, asisubiri mpaka dakika ya mwisho. Ni vyema awahi hospitalini mapema ili kupata huduma stahiki na kuepuka vifo vya mama na mtoto,” amesisitiza Anastasia.

Pia amewataka viongozi wa vijiji na vitongoji kutumia mikutano yao kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa uzazi salama hospitalini.