Micheweni FM

Vijana wahimizwa kutumia mitandao ya kijamii kwa fursa

17 November 2026, 2:10 pm

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Said Mussa Rashid akizungumzia elimu ambayo inatolewa kwa vijana juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii Picha na Essau Kalukubila.

maendeleo ya teknolojia yamefungua fursa nyingi kwa vijana ikiwemo elimu, ajira, biashara na ubunifu, hivyo ni muhimu kwao kutumia mitandao ya kijamii kwa malengo yenye tija badala ya matumizi yanayoweza kuchochea migogoro na kuvuruga amani.

Na Essau Kalukubila.

Vijana wametakiwa kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii ili kujipatia fursa mbalimbali za maendeleo zinazopatikana kupitia majukwaa hayo, sambamba na kutambua umuhimu wa kuhifadhi amani katika maeneo yao.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Said Mussa Rashid, wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa kidato cha sita na wanachuo yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Kampasi ya Pemba Amesema ni wakati wa vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa na kuepuka matumizi mabaya yanayoweza kuhatarisha amani na maendeleo ya jamii.

Sauti ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Pemba, Said Mussa Rashid

Naye mkufunzi wa mafunzo hayo ambaye pia ni Katibu wa kamati ya watumiaji wa huduma za Mawasiliano Mkoa wa kusini Pemba kutoka TCRA – CCC Khatib Bakari Kombo, amesema vijana ndio waathirika wakubwa wa matumizi yasiyo sahihi ya mitandao ya kijamii kutokana na wengi wao kutumia majukwaa hayo bila kuwa na elimu ya kutosha

Sauti ya Khatib Bakarimdau wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kiongozi wa jumuiya ya vijana

Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Jumuiya ya Vijana Pemba kwa kuwapatia elimu muhimu itakayowasaidia kutumia vyema mitandao ya kijamii na kuchangia katika kulinda amani ya nchi.

Sauti ya washiriki wa mafunzo hayo.